LYRIC

[ad_1]

Nafsi yangu

Kama vile ayala, atamanivyo,
Vijito vya maji, kule jangwani,
Hivyo nafsi yangu, yakutamani,
Kama vile walinzi, wangojeavyo,
Wangojeavyo, mapambazuko kuwadia,
(Hivyo nafsi yangu, yakungojea)X2 bwana

Jambo moja, nalitaka kwa bwana,
Nalo ndilo, nitakalolifuata
Nikae nyumbani, siku zote,
Heri kuwa mlinzi malangoni pako
Kuliko kukaa, hema la waovu,
(Uweponi mwako kuna furaha x2 timilifu

Chorus
Nafsi yangu yazikondea nyua zako
Moyo wangu na mwili yakulilia ewe bwana
Maskani yako yapendeza, nitakalolifuata mapema,
Nakuhitaji kuzidi pia X3

Kama vile jani mbali na tawi hunyauka(aaa)
Vinyo hivyo nafsi yangu ilivyo mbali nawe(mbali nawe)
Nakuhitaji X4
Nakuhitaji kuzidi pia

(Wewe ndiwe ngome yangu-ngome yangu)
Nakuhitaji kuzidi pia
Msaada wangu wa karibu-msaada wangu)
Nakuhitaji kuzidi pia
(Jiwe langu la pembeni-jiwe langux2 wee)
Nakuhitaji kuzidi pia
(Mwanga wa wokovu-wangux2bwana)
Nakuhitaji kuzidi pia
(Wewe ndiwe nguvu zangu-jabali langu yesu)
Nakuhitaji kuzidi pia

Nakuhitaji X2
Nakuhitaji kuzidi pia

[ad_2]

  1. Marcos

    August 24, 2021 at 5:40 am

    Perfect lyrics.

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ADVERTISEMENT